Psalms 10:1-6

Sala Kwa Ajili Ya Haki


1
Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bKwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?


2 cKatika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

3 Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

4 dKatika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.

5 eNjia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.

6 fAnajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”
Copyright information for SwhKC